• info@watabedigital.co.tz
  • +255 769 637 654
News Photo

Epuka Matapeli Mtandaoni, Hutuajiri Whatsapp wala Telegram

Ukuaji wa matumizi wa Mitandao ni jambo jema na kubwa katika kufanikisha mageuzi uchumi duniani pote. Matumizi salama ndiyo yatakuneemesha na matumizi yasiyosalama hayatakuacha salama. Kumbua mawasiliano sahii ya ofisi yeyote huanishwa kwenye tovuti ya ofisi husika na hayabadiliki bila sababu za msingi na iwapo yakibadilika yataainishwa tena kwenye tovuti husika.

Tabia na uelewa wa tulio wengi havishahabiani na kasi ya ukuaji na mageuzi ya kimitandao.

  • Ukosefu wa ajira umepelekea wimbi kubwa la vijana kugeuka watumwa wa mitandao wa kijamii na wangine kugeuka matapeli na watapeliwa wakudumu.

  • Tulio wengi ni wepesi wa kuamini kila tukionacho mtandaoni bila kujiridhisha.

  • Ukosefu wa taarifa sahihi na uelewa kuhusu mawasiliano sahihi ya kiofisi huchangia wengi kutapeliwa.

Madhara

  • Kutapeliwa kwa kutumia majina ya ofisi na biashara tofauti tofauti

  • kudanganywa kuhusu pesa rahisi

  • kupoteza Pesa uliyoitafuta kwa malengo fulani

  • Kutoa taarifa zako binafsi kwa watu wasio sahihi ukiwa hujui wanazishuhulikiaje kiuhalifu

 

Nini cha kufanya

  • Usiamini kila ukionacho mtandaoni bila kujiridhisha kutoka kwenye taasisi au chanzo husika

  • Usifanye muamala wowote wa kiofisi kwa mawasiliano binafsi au ambayo hayajaainishwa kwenye vyanzo vya taarifa (tovuti, mfumo) wa taasisi husika

  • Tujenge utaratibu wa kutafuta taarifa sahihi kabla ya kufanya maamuzi

  • Toa taarifa kwenye mamlaka husika kwa Tanzania uhalifu wa kimtandao unashuhulikiwa na Polisi na TCRA

  • Tuma ujumbe wa kuirepoti namba iliyohusika kukutafuta au kukutapeli kwenda 15040

Watabe Digital

Watabe Digital kama ofisi tunajivunia kutoa huduma bora kwa zaidi ya miaka saba 7 mpaka sasa. Ukuaji wa taasisi au biashara yeyote huambatana na changamoto mbalimbali. Kumekuwa na watu tofauti tofauti wakitumia majina kama Vinza Joseph, Sarah Kiongo na wengine wa jamii hiyo kuwatafuta watu kwenye mitandao ya kijamii hususani Whatsap na telegram na kujitambulisha kutokea Watabe Digital, Ukweli ni kwamba hao ni matapeli na sisi kama ofisi tumesha waripoti kwenye mamlaka husika.

Tunafanya kazi zetu kisheria na njia zetu za mawasiliano zimeanishwa kwenye tovuti yetu https://www.watabedigital.co.tz.

Sisi ni watao huduma kama ilivyoainishwa kwenye tovuti yetu hapo juu. Wasiliana nasi tukuhudumie kwa mahitaji ya Tovuti (Website), Mifumo (Systems), Seach Engine Optimization (SEO), Hosting, na Domain Names (https://www.watabedigital.co.tz/service).

Mawasiliano yetu ni:

Simu: +255 714 637 654

+255 769 637 654

+255 754 713 058

Email: info@watabedigital.co.tz

Tovuti: https://www.watabedigital.co.tz

 

Kumbuka, Mtandao ni fursa, hivyo tuutumie kwa weledi ili tubaki salama mitandaoni.

Share This News

Comment

Do you want to get our quality service for your business?